• HABARI MPYA

  Sunday, January 08, 2023

  LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA WOLVES KOMBE LA FA


  WENYEJI, Liverpool wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Raundi ya Tatu Kombe la FA jana Uwanja wa Anfield mjini Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Darwin Nunez dakika ya 45 na Mohamed Salah dakika ya 52, wakati ya Wolves yamefungwa na Goncalo Guedes dakika ya 26 na Hwang Hee-Chan dakika ya 66.
  Kwa matokeo hayo timu hizo zitarudiana Uwanja wa Molineux Stadium mjini Wolverhampton, West Midlands kutafuta nafasi ya kwenda Raundi ya Nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 NA WOLVES KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top