• HABARI MPYA

  Tuesday, January 24, 2023

  KOCHA ROBERTINHO AREJEA KWAO BRAZIL KWA WIKI


  KOCHA mpya Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ameondoka usiku wa kuamkia leo kwenda nchini kwao Brazil kwa shughuli binafsi za kifamilia.
  Taarifa ya Simba SC imesema kocha huyo aliyejiunga na timu mapema mwezi huuna atarejea nchini mwishoni mwa mwezi huu, yaani baada ya wiki moja.
  Robertinho anaondoka baada ya kuiongoza Simba kushinda mechi mbili za Ligi Kuu ya Tanzania Bara, 3-2 nyumbani dhidi ya Mbeya City na 1-0 ugenini dhidi ya Dodoma Jiji FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA ROBERTINHO AREJEA KWAO BRAZIL KWA WIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top