TIMU ya Manchester City imefanikiwa kwenda Raundi ya Tano ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal usiku huu Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Bao pekee la Man City inayofundishwa na kocha Mspaniola, Pep Guardiola limefungwa na beki wa Kimataifa wa Uholanzi, Nathan Benjamin Akes dakika ya 64 akimalizia pasi ya kiungo wa Kimataifa wa England, Jack Peter Grealish.
0 comments:
Post a Comment