• HABARI MPYA

  Thursday, January 19, 2023

  SIMBA SC YASHUSHA KOCHA MSAIDIZI KUTOKA TUNISIA


  KLABU ya Simba imemtambulisha Ouanane Sellami kuwa Kocha Msaidizi, hilo likiwa pendekezo la kocha mpya, Mbrazil Robert Oliviera ‘Robertinho’.
  Taarifa ya Simba SC jioni ya leo imesema kwamba Sellami ataungana na makocha waliopo kikosini - pamoja na Robertinho wengine ni wazawa Juma Mgunda na Suleiman Matola, kocha wa makipa, Mmorocco, Physio Faried Cassiem na Kocha wa Fiziki Kelvin Mandla Ndlomo wote kutoka Afrika Kusini. 
  Wengine katika benchi la Ufundi ni wazawa, Meneja Patrick Rweyemamu, Daktari Edwin Kagabo na Mtunza Vifaa, Hamisi Mtambo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASHUSHA KOCHA MSAIDIZI KUTOKA TUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top