• HABARI MPYA

  Monday, January 16, 2023

  YANGA SC YAICHAPA IHEFU 1-0 BAO LA MAYELE


  BAO pekee la mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 64 limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 53 katika mchezo wa 20 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tisa zaidi ya mahasimu, Simba SC waliocheza mechi 19.
  Ihefu SC baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 20 za mechi 20 sasa nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAICHAPA IHEFU 1-0 BAO LA MAYELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top