• HABARI MPYA

  Sunday, January 08, 2023

  AZAM FC YASAJILI KIPA WA KIMATAIFA WA GHANA


  KLABU ya Azam FC imemsajili kipa mahiri, Abdulai Iddrisu kwa mkataba wa miaka miwili kutoka Bechem United ya kwao Ghana.
  Usajili huo unaotokana na juhudi za mmiliki wa timu, Yusuf Bakhresa kwa pamoja na Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’ una lengo la kuboresha kikosi katika kuwania mataji ya msimu huu.
  Sasa Azam FC itakuwa na makipa wawili wa kigeni, mwingine kipa namba moja wa sasa, Mcomoro Ali Ahmada.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI KIPA WA KIMATAIFA WA GHANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top