• HABARI MPYA

  Thursday, January 19, 2023

  MCHEZAJI WA SINGIDA BIG STARS AFARIKI MAZOEZINI

  KLABU ya Singida Big Stars ile thibitisha kutokea kwa kifo cha aliyekuwa mchezaji na Nahodha wa timu yake ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Mohammed Banda, kilichotokea leo asubuhi Januari 19, 2023. 
  Banda alipoteza maisha alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya kugongana kichwani na mchezaji mwenzake wakiwa mazoezini katika Uwanja wa Magereza, Singida. 
  “Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito,” imesema taarifa ya Singida Big Stars.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHEZAJI WA SINGIDA BIG STARS AFARIKI MAZOEZINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top