• HABARI MPYA

  Friday, January 06, 2023

  MAN CITY WAICHAPA CHELSEA 1-0 STAMFORD BRIDGE


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Chelsea usiku wa Alhamisi katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa 
  1-0 Stamford Bridge Jijini London.
  Bao pekee la Manchester City lilifungwa na mshambuliaji wa Kimataifa wa Algeria, Riyad Mahrez dakika ya 63 akimalizia kazi nzuri ya kiungo wa Kimataifa wa England, Jack Grealish.
  Kwa ushindi huo, Manchester City wanafikisha pointi 39, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi tano na vinara, Arsenal baada ya wote kucheza mechi 17.
  Kwa upande wao Chelsea baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 25 za mechi 17 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY WAICHAPA CHELSEA 1-0 STAMFORD BRIDGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top