• HABARI MPYA

  Sunday, January 22, 2023

  ARSENAL YAICHAPA MANCHESTER UNITED 3-2 EMIRATES


  WENYEJI, Arsenal FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Eddie Nketiah mawili, dakika ya 24 na 90 na Bukayo Saka dakika ya 53, wakati ya Manchester United yamefungwa na Marcus Rashford dakika ya 17 na Lisandro Martínez dakika ya 59.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 50 katika mchezo wa 19 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City waliocheza mechi 20, wakati Manchester United inabaki na pointi zake 39 za mechi 20 nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA MANCHESTER UNITED 3-2 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top