• HABARI MPYA

  Sunday, January 08, 2023

  KAZADI APIGA ZOTE NNE SINGIDA YAICHAPA AZAM 4-1


  TIMU ya Singida Big Stars imetinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Azam FC usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Pongezi kwa mshambuliaji mkongwe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Francis Kazadi Kasengu aliyefunga mabao yote manne dakika za 27, 53, 64 na 86, wakati bao pekee la Azam FC limefungwa na mshambuliaji Chipukizi wa Kimataifa wa Tanzania, Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 43.
  Sasa Singida Big Stars itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho baina ya Mlandege ya Zanzibar na Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi.
  Kasengu (30), ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa aliyeanzia kuwika AS Vita, DC Motema Pembe za kwao, SCC Mohammédia na Wydad Casablanca za Morocco na Al Masry SC ya Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAZADI APIGA ZOTE NNE SINGIDA YAICHAPA AZAM 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top