• HABARI MPYA

  Friday, January 20, 2023

  MAN CITY YAIBAMIZA TOTTENHAM HOTSPUR 4-2 ETIHAD


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji, Tottenham Hotspur usiku wa jana katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Julian Alvarez dakika ya 51, Erling Haaland dakika ya 53 na Riyad Mahrez mawili dakika za 63 na 90, wakati ya Spurs yamefungwa na Dejan Kulusevski dakika ya 44 na Emerson Royal dakika ya 45.
  Kwa ushindi huo, Man City inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na vinara, Arsenal ambao pia wana mechi moja mkononi, wakati Spurs inabaki na pointi zake 33 za mechi 20 nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIBAMIZA TOTTENHAM HOTSPUR 4-2 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top