• HABARI MPYA

  Saturday, January 14, 2023

  POLISI TANZANIA YAICHAPA NAMUNGO FC 2-0 RUANGWA


  TIMU ya Polisi Tanzania imepata ushindi wa ugenini wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Mabao yote ya Polisi Tanzania leo yamefungwa na mshambuliaji wake mpya, Enock Mayala aliyesajiliwa dirisha hili dogo kutoka Sangambele ya kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Mayala alifunga dakika ya 28 na 62 akimalizia kazi nzuri ya kiungo Iddi Kipagwile na kwa ushindi huo, Polisi Tanzania wanafikisha pointi 14 katika mchezo wa 20 na kusogea nafasi ya 15, wakiizidi pointi moja Ruvu Shooting iliyocheza mechi 19.
  Kwa upande wao Namungo FC wanabaki na pointi zao 26 za mechi 20 pia nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: POLISI TANZANIA YAICHAPA NAMUNGO FC 2-0 RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top