• HABARI MPYA

  Friday, January 13, 2023

  MLANDEGE NDIO MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI 2023

  TIMU ya Mlandege ya Zanzibar imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Big Stars usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Mabao ya Mlandege yamefungwa na Bashima Saite dakika ya saba na Abdulnassir Mohamed dakika ya 17, wakati la Singida Big Stars limefungwa na Mkongo, Kazadi Kasengu dakika ya 51 ambaye amekuwa mfungaji bora kwa mabao yake sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MLANDEGE NDIO MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI 2023 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top