• HABARI MPYA

  Tuesday, January 03, 2023

  SIMBA SC YAFIKIA KUTOLEWA KOMBE LA MAPINDUZI


  BAO pekee la Abubakar Muhiddin dakika ya 75 limeipa Mlandege FC ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Simba SC katika mchezo wa Kundi C Kombe la Mapinduzi Uwanja  wa Amaan, Zanzibar.
  Kwa matokeo hayo, Simba wanavuliwa ubingwa, kwani Mlandege waliotoa droo na KVZ mechi ya kwanza tayari wana pointi nne na ndio wanakwenda Nusu Fainali kutoka kundi hilo.
  Ikumbukwe michuano ya mwaka huu ina makundi manne na kila Kundi ni mshindi wa kwanza atakayekwenda Nusu Fainali.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAFIKIA KUTOLEWA KOMBE LA MAPINDUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top