• HABARI MPYA

  Wednesday, January 18, 2023

  NTIBANZOKIZA APIGA MBILI SIMBA YAICHAPA MBEYA CITY 3-2


  WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza mawili dakika ya 11 akimalizia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama na la pili kwa penalti dakika ya 49, wakati la tatu limefungwa na winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 56.
  Mabao ya Mbeya City iliyomaliza pungufu baada ya mchezaji wake Samson Maderaka kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 65 yamefungwa na Richardson Ng’ondya dakika ya 13 na Juma Shemvuni dakika ya 78.
  Kocha mpya wa Simba, Robert Oliveira ‘Robertinho’ aliwaduwaza mashabiki wa timu hiyo baada ya kuwatoa Chama na Nahodha John Bocco dakika ya 33 na kuwaingiza Sakho na Kibu Dennis.
  Kwa ushindi wa leo Simba inafikisha pointi 47, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi sita na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 20.
  Kwa upande wao, Mbeya City nao baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 21 za mechi 20 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NTIBANZOKIZA APIGA MBILI SIMBA YAICHAPA MBEYA CITY 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top