• HABARI MPYA

  Sunday, January 29, 2023

  YANGA YAITANDIKA RHINO 7-0 NA KUSONGA MBELE ASFC


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wametinga Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na Dickson Ambundo dakika ya saba, Dickson Musonda dakik ya 16 na 46, Stephane Aziz Ki dakika ya 20, Farid Mussa dakika ya 25, Yanick Bangala dakika ya 26 na David Bryson dakika ya 90 na ushei.
  Kwa matokeo hayo, Yanga SC wanakwenda kukutana na Tanzania Prisons ambayo imeitupa nje Mashujaa FC leo kwa penalti 8-7 baada ya sare ya 2-2 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAITANDIKA RHINO 7-0 NA KUSONGA MBELE ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top