• HABARI MPYA

  Saturday, January 14, 2023

  YANGA SC YAACHANA RASMI NA YACOUBA SOGNE


  KLABU ya Yanga imeachana na mshambuliaji wake wa Kimataifa wa Burkina Faso, Yacouba Sogne (31) baada ya nyota huyo kumaliza mkataba wake.
  Sogne alikuwa nje karibu msimu wote uliopita kufuatia kuumia mguu na baada ya nusu msimu pamoja na kupata ahueni na kucheza Kombe la Mapinduzi mwezi huu, lakini klabu imetangaza kuachana naye.
  Mwenyewe Sogne ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwaaga wana Yanga; “Ulikuwa wakati mzuri tangu tulipokuwa pamoja mpaka sasa asanteni kwa upendo wenu kwangu na ushirikiano wenu kuanzia kwa wachezaji hadi uongozi wote wa yanga na mashabiki,”.
  “Daima nitawakumbuka hadi wakati mwingine wananchi asante sana na kwaherini nawapenda,” ameandika Yacouba aliyejiunga na Yanga mwaka 2020 akitokea Asante Kotoko ya Ghana baada ya awali kuchezea EF Ouagadougou, RC Kadiogo za kwao na Stade Malien ya Mali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAACHANA RASMI NA YACOUBA SOGNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top