• HABARI MPYA

  Friday, January 13, 2023

  MTIBWA SUGAR YATOA SARE 1-1 NA KMC MANUNGU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Ni Mtibwa Sugar inayofundishwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Salum Mayanga iliyotangulia kwa bao la beki, David Kameta 'Duchu' dakika ya tisa, kabla ya kiraka, Sadallah Lipangile kuisawazishia KMC dakika ya 78 kwa penalti.
  Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 25 na kusogea nafasi ya sita, wakati KMC ya kocha Mnyarwanda, Thierry Hitimana imetimiza pointi 23 nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 20.
     
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YATOA SARE 1-1 NA KMC MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top