• HABARI MPYA

  Tuesday, January 17, 2023

  AZAM FC YAICHAPA TANZANIA PRISONS 3-0 CHAMAZI


  WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa Jumatatu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na Yona Amos aliyejifunga dakika ya tano, Abdul Suleiman ‘Sopu’ na Kipre Junior dakika ya 70.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 43 katika mchezo wa 20, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja na Simba SC ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Tanzania Prisons baada ya kichapo hicho inabaki na pointi zake 21 za mechi 20 sasa nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA TANZANIA PRISONS 3-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top