• HABARI MPYA

  Saturday, January 21, 2023

  IHEFU YAICHAPA TANZANIA PRISONS 2-1 SOKOINE


  TIMU ya Ihefu SC imepata ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Ihefu kutoka Mbarali, Ubaruku mkoani Mbeya yamefungwa na Ezekia Mwashilindi aliyejifunga dakika ya pili na Raphael Daudi Lothi dakika ya 90, wakati la Tanzania Prisons limefungwa na Jeremiah Juma dakika ya 64.
  Kwa matokeo hayo, Ihefu inafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya 10, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake pointi 21 na kushukia nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU YAICHAPA TANZANIA PRISONS 2-1 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top