• HABARI MPYA

  Saturday, January 07, 2023

  YANGA YATUPWA NJE KOMBE LA MAPINDUZI BAADA YA SARE NA SINGIDA


  VIGOGO, Yanga wametupwa nje ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya sare ya 1-1 na Singida Big Stars katika mchezo wa Kundi B leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Singida Big Stars walitangulia kwa bao la nyota wao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Francis Kazadi Kasengu dakika ya 22, kabla ya beki David Bryson kuisawazishia Yanga dakika ya 31.
  Kwa matokeo hayo, timu zote zinamaliza na pointi nne, lakini Singida Big Stars wanakwenda Nusu Fainali kwa kuizidi Yanga bao moja.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YATUPWA NJE KOMBE LA MAPINDUZI BAADA YA SARE NA SINGIDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top