• HABARI MPYA

  Sunday, January 22, 2023

  BALEKE AING’ARISHA SIMBA SC DODOMA, YASHINDA 1-0


  BAO pekee la mshambuliaji mpya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean Toria Baleke Othos limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Baleke aliyesajiliwa kwa mkopo kutoka TP Mazembe ya kwao, Lubumbashi baada ya msimu uliopita kucheza kwa mkopo pia Nejmeh SC ya Lebanon alifunga bao hilo dakika ya 45 na ushei akitumia makosa ya kipa wa Dodoma Jiji na walinzi wake.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 50 katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Dodoma Jiji wanabaki na pointi zao 21 za mechi 21 sasa nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALEKE AING’ARISHA SIMBA SC DODOMA, YASHINDA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top