• HABARI MPYA

  Sunday, January 15, 2023

  SIMBA SC YASAJILI KIUNGO MBURKINABE KUTOKA MOROCCO


  KLABU ya Simba imemtambulisha kiungo wa ulinzi wa Kimataifa wa Burkina Faso, Hamed Ismael Sawadogo kuwa mchezaji wake mpya katika dirisha hili dogo.
  Sawadogo anakuwa mchezaji mpya wa pili katika dirisha hili dogo baada ya kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi, Saido Ntibanzokiza aliyekuwa anacheza Geita Gold.
  Sawadogoni (26) anajiunga na Simba kutoka Difaâ El Jadida ya Morocco baada ya awali kuzitumikia Enppi SC ya Misri, Al-Arabi SC ya Kuwait, Al Mabarra ya Lebanon, AS Douanes, US Ouagadougou, Salitas na RC Kadiogo za kwao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI KIUNGO MBURKINABE KUTOKA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top