• HABARI MPYA

  Friday, January 27, 2023

  AZAM FC YAITANDIKA DODOMA JIJI 4-1 NA KUSONGA MBELE ASFC


  TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na Edward Charles Manyama dakika ya 10, Daniel Amoah dakika ya 27, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 47 na Justin Bilal aliyejifunga dakika ya 51, wakati la Dodoma Jiji limefungwa na Muhsin Makame dakika ya 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAITANDIKA DODOMA JIJI 4-1 NA KUSONGA MBELE ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top