• HABARI MPYA

  Thursday, January 26, 2023

  MAN UNITED YATANGULIZA MGUU FAINALI CARABAO CUP

   


  TIMU ya Manchester United imetanguliza mguu mmoja katika Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest usiku wa jana Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire.
  Katika mchezo huo wa Nusu Fainali ya kwanza, mabao ya Manchester United yamefungwa na Marcus Rashford dakika ya sita, Wout Weghorst dakika ya 45 na Bruno Fernandes dakika ya 89.
  Timu hizo zitarudiana Februari 1 Uwanja wa Old Trafford na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Southampton na Newcastle United. Mechi ya kwanza Newcastle ilishinda 1-0 ugenini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATANGULIZA MGUU FAINALI CARABAO CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top