• HABARI MPYA

  Sunday, January 15, 2023

  SIMBA YASAJILI MSHAMBULIAJI MKONGO JEAN BELEKE KUTOKA LEBANON


  KLABU ya Simba imemtambulisha mshambuliaji Mkongo, Jean Toria Baleke Othos (21) kutoka Nejmeh SC ya Lebanon kuwa mchezaji wake mwingine mpya katika dirisha hili dogo.
  Beleke anayesajiliwa katika siku ya mwisho ya kufunga pazia, anakuwa mchezaji mpya wa tatu dirisha hili dogo baada ya kiungo wa ulinzi Mburkinabe, Hemed Ismael Sawadogo kutoka Difaa El Jadida ya Morocco na kiungo mshambuliaji Mrundi, Saido Ntibanzokiza kutoka Geita Gold.
  Kabla ya kwenda Lebanon Agosti mwaka jana tu, Beleke alicheza TP Mazembe kuanzia Januari mwaka 2021 baada ya kuibukia klabu ya JS Kinshasa zote za kwao, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YASAJILI MSHAMBULIAJI MKONGO JEAN BELEKE KUTOKA LEBANON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top