• HABARI MPYA

  Monday, January 23, 2023

  YANGA SC YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 BAO LA KUJIFUNGA


  BAO la kujifunga la Nahodha wa Ruvu Shooting, Mpoki Mwakinyuke limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, mabingwa hao watetezi wanafikisha pointi 56 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya mahasimu, Simba SC baada ya wote kucheza mechi 21.
  Kwa upande wao Ruvu Shooting hali inazidi kuwa mbaya wakiendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 wakibaki na pointi zao 14 za mechi 21 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 BAO LA KUJIFUNGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top