• HABARI MPYA

    Tuesday, January 05, 2021

    MTIBWA SUGAR WAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI BAADA YA KUIPIGA CHIPUKIZI 1-0 UWANJA WA AMAAN

    BAO pekee la Ibrahim Ahmada 'Hilika' dakika ya 58 limewapa mwanzo mzuri mzuri mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Chipukizi kwenye mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi jioni ya leo Uwanja wa Amaan.
    Mechi ya Kundi A baina ya vigogo Yanga SC na Jamhuri ya Pemba inafuatia Saa 2:30 usiku Uwanja wa Amaan.
    Kwa ujumla, Kundi A kuna Yanga SC, Namungo FC ya Lindi na Jamhuri FC ya Pemba, Kundi B kuna Simba SC, Mtibwa Sugar na Chipukizi FC na Kundi C kuna Azam FC, Malindi FC na Mlandege FC.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTIBWA SUGAR WAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI BAADA YA KUIPIGA CHIPUKIZI 1-0 UWANJA WA AMAAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top