BEKI timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Azam FC, Shaaban Kingazi akiwa safarini kuelekea nchini England kwa mwaliko wa Nahodha wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya England, Dennis Wise kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Kingazi amepata nafasi huyo ambayo itampa fursa ya kufanya majaribio katika timu mbalimbali nchini humo baada ya kuwa miongoni mwa vijana waliopatikana katika kliniki ya uvumbuaji wa vipaji vya soka kwa vijana wadogo iliyoendeshwa na kampuni ya Cambiasso Sports ikishirikiana na Rainbow Sports.
0 comments:
Post a Comment