• HABARI MPYA

  Sunday, January 01, 2023

  COASTAL UNION YATOA SARE 1-1 NA NAMUNGO FC MKWAKWANI


  WENYEJI, Coastal Union wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Ni Namungo waliotangulia kwa bao la Ibrahim Abdallah dakika ya 47, kabla ya Maabad Maulid kuisawazishia Coastal Union kwa penalti dakika ya 60.
  Kwa matokeo hayo kwa mchezo wa 19 kwa kila timu, Coastal Union wanafikisha pointi 17, ingawa wanabaki nafasi ya 14, wakati Namungo inafikisha pointi 26 na inabaki nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YATOA SARE 1-1 NA NAMUNGO FC MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top