• HABARI MPYA

  Sunday, January 01, 2023

  YANGA SC YAMTOA KWA MKOPO MSHAMBULIAJI WAKE


  MSHAMBULIAJI Yusuph Athumani amejiunga na Coastal Union ya Tanga hadi mwisho wa msimu kwa mkopo kutoka Yanga SC.
  “Nyota wetu, Yusuph Athuman ameomba kutolewa kwa mkopo ili apate muda zaidi wa kucheza baada ya ushindani wa namba kuwa mkubwa kwenye kikosi cha Yanga,” imeeleza taarifa ya Yanga SC.
  Athuman alijiunga na Yanga akitokea Biashara United FC ya Mara msimu wa 2021-2022, bahati mbaya kwake hakupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na kushindwa kumshawishi kocha Mtunisia, Nasredine Nabi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAMTOA KWA MKOPO MSHAMBULIAJI WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top