• HABARI MPYA

  Saturday, December 31, 2022

  ARSENAL YAIBUTUA BRIGHTON 4-2 THE AMEX


  VINARA wa Ligi Kuu ya England, Arsenal wameuaga mwaka 2022 kwa ushindi wa ugenini wa 4-2 dhidi ya Brighton & Hove Albion leo Uwanja wa The AMEX, East Sussex.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Bukayo Saka dakika ya pili, Martin Odegaard dakika ya 39, Eddie Nketiah dakika ya 47 na Gabriel Martinelli dakika ya 71, wakati ya Brighton yamefungwa na Kaoru Mitoma dakika ya 65 na kinda wa miaka 18, Evan Ferguson dakika ya 77.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 43 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi saba zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City, wakati Brighton inabaki na pointi zake 24 za mechi 16 nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAIBUTUA BRIGHTON 4-2 THE AMEX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top