• HABARI MPYA

  Thursday, September 09, 2021

  ITALIA YASHIDA 5-0 KUFUZU KOMBE LA DUNIA

  MSHAMBULIAJI wa Juventus, kinda wa miaka 21, Moise Bioty Kean amefunga mabao mawili dakika ya 11 na 29, Italia ikiibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Lithuania katika mchezo wa Kundi A kufuzu Kombe la Dunia Uwanja wa MAPEI - Città del Tricolore mjini Reggio nell'Emilia.
  Mabao mengine ya Italia yamefungwa na kiungo wa Cercle Brugge, Edgaras Utkus aliyejifunga dakika ya 14, mshambuliaji wa Sassuolo, Sassuolo Raspadori dakika ya 24 na beki wa Napoli, Giovanni Di Lorenzo dakika ya 54.
  Kwa ushindi huo, Azzuri inafikisha pointi 13 na kundelea kuongoza Kundi A kwa pointi mbili zaidi ya Serbia baada ya mechi tano.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ITALIA YASHIDA 5-0 KUFUZU KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top