• HABARI MPYA

  Saturday, September 18, 2021

  GOMES: MAZEMBE KIPIMO KIZURI

   KOCHA wa Simba SC, Mfaransa Didier Gomes Da Rosa amesema mechi dhidi ya TP Mazembe kesho itakuwa kipimo kizuri kwa kikosi chake kabla ya msimu mpya. 
  Tayari mabingwa mara nne Afrika, TP Mazembe wamewasili mchana wa leo Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kutoka Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya mchezo huo kwenye tamasha la Simba Day kesho jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini.
  “Itakuwa siku nzuri sababu tunaenda kukutana na mashabiki wetu baada ya muda kupita. Tunaishukuru TP Mazembe kwa kukubali kucheza na sisi Simba Day. Ni moja ya timu bora Afrika na tutacheza kwa heshima kubwa ili tushinde mchezo huu,” amesema Kocha Gomes akizungumza na Waandishi wa Habari leo. 


  Kwa upande wake, Nahodha wa Simba, John Raphael Bocco “itakuwa ni mechi nzuri kwao ya kujipima kuelekea msimu mpya. 
  "Kama wachezaji tuko tayari kuwaonyesha tulivyojiandaa kwa msimu mpya. Tumejiandaa kuwafurahisha mashabiki wetu, hivyo tunawaomba wajitokeze kwa wingi kuja kuona tulivyojipanga," amesema Kapteni Bocco.
  Wakati huo huo: Uongozi wa Simba SC kwa kushirikiana na Taasisi ya Mo Dewji Foundation umetoa msaada wa vitanda, magodoro, vipimo vya ugonjwa wa shinikizo la damu na vitanda vya kujifungulia wajawazito katika hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo Zanzibar.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GOMES: MAZEMBE KIPIMO KIZURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top