• HABARI MPYA

  Thursday, September 16, 2021

  MAN CITY WASHINDA 6-3 ETIHAD

  TIMU ya Manchester City imeibuka na ushindi wa 6-3 dhidi ya RB Leipzig katika mechi yao ya kwanza ya Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Etihad.
  Mabao ya Man City yamefungwa na Nathan Ake dakika ya 16, Nordi Mukiele aliyejifunga dakika ya 28, Riyad Mahrez kwa penalti dakika ya 45, Jack Grealish dakika ya 56, João Cancelo dakika ya 75 na Gabriel Jesus dakika ya 85, wakati ya RB Leipzig yote yalifungwa na Christoph Nkunku dakika ya 42, 51 na 73.
  Pamoja na kipigo hicho, beki wa zamani wa Man City, Angelino alitolewa kwa kadi nyekundu 79 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY WASHINDA 6-3 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top