• HABARI MPYA

  Saturday, September 11, 2021

  CAF YAZUIA MASHABIKI MECHI YA YANGA


   SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limezuia watazamaji katika mechi ya kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Yanga SC na Rivers United ya Nigeria kesho.
  Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo, CAF imezuia watazamaji katika mechi zote za Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa zinazochezwa Tanzania.
  Yanga SC watakuwa wenyeji wa Rivers United kesho Saa 11:00 jioni katika mechi ya kwanza ya Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 19 Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YAZUIA MASHABIKI MECHI YA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top