• HABARI MPYA

  Thursday, September 23, 2021

  GYNAH KATIKA USIKU WA KAHAWA

  MSANII chipukizi katika fani ya Muziki, Mavazi na Filamu, Regina Beraldo Kihwele a.k.a (Gynah) anatarajia kutambulisha Kazi zake za Sanaa zenye kubeba jina la "USIKU WA KAHAWA(COFFEE NIGHT)" tarehe 24/09/2021 katika Ukumbi wa Little Theatre jijini Dar Es Salaam.
  Katika maonesho hayo  kutakuwa na kazi za Uchoraji, ubunifu wa Mavazi, picha za kuchora, pamoja na uzinduzi wa nyimbo zake 5 mpya kwa mashabiki wake.
  Aidha, Regina (Gynah) ambaye amesajiliwa na BASATA, ameteuliwa kuwania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike (Best Actress) kupitia LIPFF FESTIVAL 2021  Afrika ambapo Tuzo hizo zitafanyika mwishoni mwa mwaka huu 2021 nchini Kenya.
  Tuzo hizi  zinashindaniwa na Wasanii wengine kutoka Afrika ya Kusini, Cameroon, Uganda, Tanzania na Morocco.
  Tuzo hizi zinafadhiliwa na wadau kutoka Legacy Arts and film Lab na Lake International Pan-african Film Festival.
  Hivi karibuni Regina (Gynah) ameshiriki pia katika Filamu ijulikanayo "Mulasi" chini ya Muongozaji na Mtayarishaji wa Filamu mahiri kutoka  Riccobs Ent. Bi. Honeymoon Aljabri, Mtanzania anayeishi nchini Marekani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GYNAH KATIKA USIKU WA KAHAWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top