• HABARI MPYA

  Saturday, September 18, 2021

  BALOZI NIGERIA ‘AWAPA MOYO’ YANGA


  BALOZI wa Tanzania nchini Nigeria, DK. Benson Bana akizungumza na kocha wa Yanga SC, Mtunisia Nasreddine Nabi leo Jijini Port Harcourt alipoitembelea timu hiyo kuelekea mechi ya marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Rivers United kesho Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini humo.

  Nahodha wa Yanga SC, Bakari Nondo Mwamnyeto akizungumza kwa niaba ya wachezaji kufuatia hotuba ya Balozi Dk. Benson Bana.


  Yanga SC wanatakiwa kushinda angalau 2-0 ili kusonga mbele baada ya kuchapwa 1-0 Jumapili iliyopita katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.  Kama Yanga wataweza na wao kushinda 1-0 ugenini, mchezo utaamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALOZI NIGERIA ‘AWAPA MOYO’ YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top