• HABARI MPYA

  Thursday, September 23, 2021

  KAYOKO REFA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI


  REFA chipukizi, Ramadhani Kayoko atachezesha mechi ya Ngao ya Jamii baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kayoko aliyechezesha mechi ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) mwaka juzi Simba ikishinda 4-1, keshokutwa atasaidiwa na Frank Kombe na Soud Lila wote wa Dar es Salaam.
  Katika mchezo uliofanyika Julai 12, mwaka 2020, mabao ya Simba yalifungwa na viungo Mbrazil Gerson Fraga ‘Viera’ dakika ya 21, Mzambia Clatous Chama dakika ya 50, Luis Miquissone wa Msumbiji dakika ya 52 na Muzamil Yassin dakika ya 89, wakati la Yanga lilifungwa na kiungo pia, Feisal Salum dakika ya 70.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAYOKO REFA SIMBA NA YANGA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top