• HABARI MPYA

  Tuesday, September 14, 2021

  MWANAHAMISI OMARY AJIUNGA NA TWIGA STARS

   MSHAMBULIAJI wa Chabab Atlas Khenifra ya Morocco, Mwanahamisi Omary Shaluwa ‘Gaucho’ amewasili Dar es Salaam jana kujiunga na timu ya taifa, Twiga Stars inayojiandaa na mashindano ya COSAFA na kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (AFCON).
  Katika michuano ya COSAFA Tanzania imepangwa Kundi B pamoja na Zimbabwe, Botswana na Sudan Kusini, wakati kufuzu AFCON ya mwakani Morocco watacheza na Namibia.
  Twiga Stars wataanza michuano ya COSAFA kwa kumenyana na Zimbabwe Septemba 16 Jijini Gqeberha, zamani Port Elizabeth, kabla ya kuivaa Botswana Septemba 19 na kukamilisha mechi za kundi hilo kwa kumenyana na Sudan Kusini Septtemba 21.


  Aidha, timu ya taifa ya vijana ‘Tanzanites’ nayo itacheza na Eritrea ikianzia ugenini wiki ijayo, kabla ya kurudiana hapa Dar es Salaam wiki moja baadaye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWANAHAMISI OMARY AJIUNGA NA TWIGA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top