• HABARI MPYA

  Wednesday, September 29, 2021

  PACQUIAO AJIUZULU NGUMI BAADA YA MIAKA 26

  GWIJI  wa ngumi, Manny Pacquiao ametangaza kustaafu mchezo huo baada ya miaka 26 ulingoni akicheza mapambano 72 na kushinda mataji 12.
  Hatua hiyo inakuja mwezi mmoja tangu apoteze pambano mbele ya Mcuba, Yordenis Ugas kwa pointi Jijini Nevada Agosti 21, mwaka huu.
  Pacquiao ambaye ameshinda mapambano 62, kati ya hayo 39 kwa Knockouts (KO), akipigwa nane na kutoa sare mawili ni bondia pekee kihistoria kushinda mataji ya dunia katika madaraja nane tofauti.


  Seneta huyo wa Ufilipino, sasa anatarajiwa kuelekeza nguvu zake zaidi kwenye siasa baada ya kutangaza kuwania Urais wa nchi yake mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PACQUIAO AJIUZULU NGUMI BAADA YA MIAKA 26 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top