• HABARI MPYA

  Sunday, September 12, 2021

  EMMA RADUCANU BINGWA US OPEN

  BINTI Muingereza, Emma Raducanu amekamilisha historia baada ya kutwaa taji la michuano ya Tenisi ya US Open kufuata kumchapa Leylah Fernandez seti 2-0 (6-4, 6-3) hilo likiwa taji lake la kwanza la Grand Slam.
  Tayari Raducanu alishaweka historia baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kuanzia kwenye hatua ya mchujo hadi kufika fainali ya michuano tangu mwaka 1968.
  Binti huyo wa umri wa miaka 18 anakuwa bingwa mdogo zaidi wa Grand Slam tangu Maria Sharapova alipotwaa taji la Wimbledon mwaka 2004 akiwa ana umri wa miaka 17.

  Akishiriki michuano yake ya pili tu ya Grand Slam, Raducanu pia ameweka rekodi ya mchezaji wa kwanza tangu Serena Williams mwaka 2014 kutopoteza seti katika US Open akiwatoa wachezaji watatu wa Tano Bora hadi kufika fainali.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EMMA RADUCANU BINGWA US OPEN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top