• HABARI MPYA

    Friday, September 10, 2021

    BIASHARA UNITED YASHINDA 1-0 DJIBOUTI

    TIMU ya Biashara United imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, FC Dikhil katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa El Hadj Hassan Gouled Jijini Ville de Djibouti nchini Djibouti.
    Bao pekee la Biashara United katika mchezo huo limefungwa na beki Denis Nkane dakika ya 52 na sasa timu hizo zitarudiana Septemba 18 Dar es Salaam.
    Mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Hay Alwady Nyala ya Sudan na Al Ahli Tirpoli ya Libya.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BIASHARA UNITED YASHINDA 1-0 DJIBOUTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top