• HABARI MPYA

  Saturday, September 18, 2021

  YANGA SC WAWASILI SALAMA PORT HARCOUT

  KIKOSI cha Yanga kimewasili salama Jijini  Port Harcourt nchini Nigeria tayari kwa mchezo  dhidi ya wenyeji, Rivers United kesho.
  Yanga watakuwa wageni wa Rivers kesho katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United Jumapili Saa 12:00 jioni Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini  Port Harcourt.
  Yanga SC waliokwenda kwa ndege ya kukodi ya ATCL ambayo itawasubiri hadi baada ya mechi kesho na kurejea nao nchini – wanatakiwa kushinda 2-0 ili kusonga mbele kufuatia kuchapwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza  Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 


  Na kama watashinda 1-0 mchezo utaamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti na mshindi wa jumla atakutana na mshindi kati ya Fasil Kenema Ethiopia na Al Hilal ya Sudan.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAWASILI SALAMA PORT HARCOUT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top