• HABARI MPYA

  Wednesday, September 29, 2021

  YANGA YAANZA VYEMA LIGI KUU


  BAO pekee la kiungo Mzanzibari, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ dakika ya 24 limeipa mwanzo mzuri Yanga SC katika Ligi a Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Kagera Sugar 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.
  Fei Toto amefunga bao hilo kwa shuti la mguu wa kushoto akimalizia mpira uliookolewa na kipa Issa Chalamanda kufuatia shuti la awali la mshambuliaji Mkongo, Fiston Mayele Kalala.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, mabao ya mshambuliaji Vitalis Mayanga dakika ya tatu na 20 yameipa Polisi Tanzania ushindi wa 2-0 dhidi ya KMC Uwanja wa Black Rhino, Karatu mkoani Arusha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAANZA VYEMA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top