• HABARI MPYA

  Friday, September 17, 2021

  YANGA SC WAIFUATA RIVERS UNITED


  KIKOSI cha Yanga kimeondoka jioni ya kwenda Nigeria kwa ajili ya mechi ya marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Rivers United Jumapili Uwanja wa Adokiye Amiesimaka Jijini Port Harcourt, Nigeria.
  Yanga SC wanatakiwa kushinda angalau 2-0 ili kusonga mbele baada ya kuchapwa 1-0 Jumapili iliyopita katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kama Yanga wataweza na wao kushinda 1-0 ugenini, mchezo utaamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC WAIFUATA RIVERS UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top