• HABARI MPYA

    Thursday, September 30, 2021

    LEWANDOWSKI APIGA MBILI, BAYERN YASHINDA 5-0


    WENYEJI, Bayern Munich wameibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya Dynamo Kyiv katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, Ujerumani.
    Mabao ya Bayern Munich jana yalifungwa na Robert Lewandowski mawili, dakika ya 12 na 27 akimalizia pasi ya Thomas Müller, Serge Gnabry dakika ya 68, Leroy Sané dakika ya 74 na Erick Choupo-Moting dakika ya 87.
    Ushindi huo unawafanya Bayern Munich waendelee kuongoza Kundi E wakifikisha pointi sita, mbele ya Benfica wenye pointi nne, Dinamo Kiev pointi moja na Barcelona ambayo haina pointi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LEWANDOWSKI APIGA MBILI, BAYERN YASHINDA 5-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top