• HABARI MPYA

  Wednesday, September 22, 2021

  LEWANDOWSKI AKABIDHIWA KIATU CHA DHAHABU


  NYOTA wa Bayern Munich, Robert Lewandowski jana amekabidhiwa tuzo ya Kiatu cha Dhahabu Ulaya 2021  baada ya kuwa mfungaji bora wa bara hilo msimu uliopita 2020/21.
  Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Poland, Lewandowski alifunga mabao 41 katika mechi 29 za Bundesliga akifuatiwa na Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
  Wakati Muargentina, Messi alifunga mabao 30 akiwa Barcelona kwenye La Liga, Mreno Cristiano Ronaldo alifunga mabao 29 akiwa Juventus katika Serie A.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LEWANDOWSKI AKABIDHIWA KIATU CHA DHAHABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top