• HABARI MPYA

  Thursday, September 23, 2021

  YANGA YAICHAPA DTB 3-1 KIGAMBONI

  KATIKA kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii utakaofanyika Jumamosi, Yanga jana ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Daraja la Kwanza, DTB na kuibuka na ushindi wa 3-1.
  Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Avic Town, Somangira, Kigamboni Jijini Dar es Salaam na mabao ya Yanga yalifungwa na beki David Bryson na washambuliaji Yussuf Athumani na Mkongo, Fiston Kalala Mayele.
  Yanga watamenyana na Simba Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa Ngao ya Jamii kuanzia Saa 1:00 usiku.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAICHAPA DTB 3-1 KIGAMBONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top