• HABARI MPYA

  Saturday, September 18, 2021

  BIASHARA YASONGA MBELE KOMBE LA SHIRIKISHO

  MABAO ya kiungo mkongwe, Ramadhani Suleiman Chombo 'Redondo' dakika ya 19 na 23 yameipa ushindi wa 2-0 Biashara United dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Kwa matokeo hayo, Biashara inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Djibouti City wiki iliyopita na sasa itakutana na mshindi kati ya Hay Alwady Nyala ya Sudan na Al Ahli Tirpoli ya Libya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA YASONGA MBELE KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top